Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » MAPAMBANO MAKALI YAZUKA KATI YA POLISI NA CHADEMA. ANGALIA HALI ILIVYOKUWA HUKO MKOANI MWANZA!

MAPAMBANO MAKALI YAZUKA KATI YA POLISI NA CHADEMA. ANGALIA HALI ILIVYOKUWA HUKO MKOANI MWANZA!

Maandamano ya chama cha CHADEMA yaliyokua yanafanyika huko mwanza yamegeuka vurugu baada ya wandamanaji kuanza kupambana na polisi.

CHADEMA walikua wakiandamana katika kushinikiza Meya wa Ilemela Henry Matata aachie ngazi kwani hana sifa zakua meya, baada ya kuvuliwa uanachama na chama hicho.

Katika picha zilizokirushwa kupitia televisheni ya Barmedas Tv ya Mwanza,  barabara zimeonekana zikiwa zimefungwa kwa mawe na miti, huku  katika maeneo mengine uchafu ukiwa umejazwa barabarani na matairi kuchomwa.

katika mtaa wa Mission waandamanaji wamefunga barabara kwa uchafu uliokua katika dampo moja kando ya barabara hiyo.

Maandamoano hayo yalikua yamalizikie viwanja vya furahisha ambapo viongozi wa chadema walikua wahutubie.

Chanzo cha vurugu hizo hakijafahamika, ikizingatiwa CHADEMA walikua na kibali cha kufanya maandamano hayo.

Hivi sasa polisi wametanda mitaani katika kudhibiti vurugu hizo na hali inaonekana kutengamaa.

PICHA ZAIDI NI HIZI HAPA...

Wakazi wa Mwanza wakiwa kwenye Maandamano kwaajili ya Kumng'oa Meya wa Ilemela huku wakisindikizwa na Askari wa Kutuliza Ghasia
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa