Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » "CHUKI KWA WASANII WA BONGO MUVI INATOKANA NA KUCHUKILIANA MABWANA"-BATULI

"CHUKI KWA WASANII WA BONGO MUVI INATOKANA NA KUCHUKILIANA MABWANA"-BATULI

MWIGIZAJI wa kike wa filamu Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amefunguka kwa kuongelea ugomvi na chuki ambazo zimekuwa zikiripoti kwa akina dada kutoka Bongo movie sababu kubwa ni ugomvi wa kuibiana wanaume mapedeshee ambao wamekuwa wakiwaweka mjini kwa kuwapangia majumba na kuwapatia magari wakitanua nayo mjini.

“Chuki yetu wasanii wa Bongo movie ni kuchukuliana mabwana yaani mtu ukiwa na mtu anayekusaidia huwezi kabisa kumtambulisha kwa shoga yako kwani ukimpa mgongo tu si wako huyo tena, naongea bila uoga tunahitaji maisha mazuri lakini filamu hazilipi hivyo ukiona msanii wa kike anafanya kitu lazima ujue nyuma yake kuna mtu na si kwa ajili ya malipo ya filamu ni mapedeshee hao,”
anasema Batuli.

Lakini pia Batuli anawalaumu sana wasanii wenzake wa kike kwa kukosa ubunifu na kutotumia fursa wanazopata kutoka sehemu mbalimbali hata serikali pia, msanii huyo amedai kuwa kuna msanii aliwahi hata kupata mwariko kwa rais wa nchi nyingine lakini kutokana na uwezo wake wa kutokufiri hakwenda kuonana na rais, hivyo Batuli anasisitiza kuwa hakuna msanii wa kike anayeweza kusimama kama yeye zaidi ya kuwategemea mapedeshee waliojificha nyuma yao

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa