Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » HUU NDIO UJUMBE MZITO WA RAY c KWENDA KWA JAMII

HUU NDIO UJUMBE MZITO WA RAY c KWENDA KWA JAMII

Rehema Chalamila the award winning singer ambaye aliathirika na matumizi ya dawa za kulevya na baadae kupona. Ameendelea kuwa kioo cha jamii kwa ku-share experience yake baada ya kupona kwenye ishu ya dawa za kulevya. Ray C ametoa ujumbe mpya ambao ni muhimu kila mtu kuujua kwasababu kwenye mazingira yetu kuna waathirika wengi wa dawa za kulevya.
Haya ndiyo maneno ya Ray C mwenyewe ambayo yana ujumbe mzuri ndani yake:

“Wote hawa tuliokaa hapa(picha hapo chini) tuliathirika na dawa za kulevya na tumepona kwa kunywa dawa moja tu inayoitwa Methadone. Inapatikana Muhimbili na Mwananyamala pekee na ni bure kabisa.
Tunamshukuru sana Mh Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutuletea dawa hii.Ningependa kuwashauri walioathirika wa dawa za kulevya iwe wewe,ndugu yako,rafiki,kaka,dada,mjomba,jirani au yoyote aliye karibu na wewe.Usiogope amua tu kwamba unataka kupona na nenda kanywe hii dawa utapona kabisa.”
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa