Msichana  mmoja ambaye jina lake halikujulika amejikukuta katika wakati mgumu  baada ya kuzomewa na   kuchapwa viboko na kundi la watu katika eneo la  soko la nmc jiji arusha kwa madai ya kuvaa nguo fupi hali iliyowalazimu  wasamariawema kuingilia kati  na kutumia nguvu kubwa ili  kumwokoa na  kumsitili kwa kumfunika na nguo zingine.
 Mwandishi wetu Halfani Lihundi  kutoka arusha  alikuwapo katika sakata hilo na ametuma taarifa hii iliyosema,  watu  walio shuhudia tukio hilo wamesema wamechukizwa na aina ya nguo  alizizovaa msichana huyo ambazo haziendani na maadili ya Kitanzania,  ndiyo maana wameamua kumwadabisha ili kukomesha tabia hiyo.
Kwa upande wao wanawake waliyo msitili msichana huyo  kwa kumpa nguo za heshima na kumhifadhi katika Gareji ya jirani kabla ya  kumkimbiza kwa gari aina ya Toyota Hiace wamesema hawaridhishwi na  tabia hiyo inayowazalilisha wanawake na kuwataka wasichana kuavaa nguo  za kujisitili ili kujenga heshima katika jamii.
  -ITV

 

 
 
 
 
 
