Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » MWANAMKE ALIYEACHANA NA MUMEWE ACHARANGWA MAPANGA KISA NI KUTAKA KUGAWANA MALI NA MUMEWE

MWANAMKE ALIYEACHANA NA MUMEWE ACHARANGWA MAPANGA KISA NI KUTAKA KUGAWANA MALI NA MUMEWE

Mwanamke mmoja Sumayi Girandi mkazi wa kijiji cha Kunzugu wilayani Bunda amepoteza vidole vitatu vya mkono wa kulia na kiganja cha mkono wa kushoto kukatwa baada kushambuliwa kwa mapanga na watu wasiojulikana kisa kikidaiwa kuwa kutaka kunyang’anywa mali zake.

Uhodari wa mama huyo wa kutafuta mafanikio ya familia yake hasa baada ya kutengana na mume wake umeishia hapo baada ya watu wasiojulikana kumvamia nyumbani kwake na kumshambulia kwa mapanga na hiyo haitoshi wakamkata kiganja cha mkono wa kushoto kuanguka.

Kwa sasa Sumayi Girandi anatibiwa katika Hospitali teule ya wilaya lakini pamoja na kujeruhiwa kote huko hakusita kuzungumza na TBC juu ya hayo yaliyomkuta.

Vitendo vya kujeruhi na kuua wanawake mkoani Mara kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ya ndugu kutaka kuwanyang’anya bado vinaendelea.

Katika tukio lingine wilayani Bunda dereva mmoja wa pikipiki ameuawa na watu wasiojulikana ambapo taarifa zinasema kuwa kabla ya kuuawa kwa dereva huyo wa bodaboda inadaiwa alikodiwa na watu wawili.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mara Ferdinand Mtui amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na tayari watu wanne wamekamatwa wakiwemo watu wanaotuhumiwa kumkatakata mapanga mwanamke Sumayi Girandi.
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa