Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » , » "SIACHI MKOROGO HADI MADUKA YAFUNGWE"...WEMA SEPETU

"SIACHI MKOROGO HADI MADUKA YAFUNGWE"...WEMA SEPETU

THE big boss wa The Endless Fame Production, Wema Isaac Sepetu ametundika mtandaoni picha zinazoonesha mapaja yake jinsi yalivyoharibika na kuweka michirizi ambapo alipoulizwa na shushushu wetu kulikoni, alisema kuwa hataacha mkorogo hadi maduka yafungwe.
 
Wema katika pozi linaloonesha mapaja yake jinsi yalivyoharibika.
Baada ya staa huyo wa filamu za ‘kikwetukwetu’ kuulizwa na kujibu hivyo wikiendi iliyopita, alitundika picha nyingine kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa BBM zikimuonesha akiwa nyumbani kwake, Kijitonyama jijini Dar huku madhara ya mkorogo yakionekana waziwazi kwenye mwili wake.
 
..Mapaja ya mrembo huyo.
Baadhi ya marafiki zake walianza kujadili namna alivyoharibika na wengine kudai matumizi ya vipodozi vikali maarufu kwa jina la mkorogo ndiyo vimemfanya apasuke kiasi hicho.

Wema, baada ya kupokea maoni mengi juu ya picha hizo mengine yakiwa ni ya kejeli, aliwajibu kwa kuandika kuwa hataacha matumizi ya mkorogo hadi maduka yanayouza yafungwe.
Wema alipotafutwa  ili aweze kuweka wazi madai haya hakutoa ushirikiano kufuatia simu yake ya kiganjani kuita muda wote bila kupokelewa.

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa