Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Barack Obama wakipokea saluti wakati nyimbo za Taifa zikipigwa ,wakati wa kuondoka kwa Rais huyo wa Marekani leo katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julias Nyerere .
Nyuma yao ni mama Salma Kikwete na mama Michelle Obama pamoja na mkuu wa majeshi Davis Mamunyange pamoja na IGP Said Mwema .
Kushoto ni mkuu wa itifaki Balozi Mohamed Maharage na mkuu wa itifaki wa ikulu ya Marekani ( white House ) balozi capricia Marshall..Ziara ya Rais Obama inatajwa kuwa moja kati ya ziara za viongozi wan je zilifanikiwa sana, ambapo pia maelfu ya Watanaznia waljitokeza kumlaki na kumuaga.
![]() |
Rais Barack Obama akiagama na mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam huku Mstahiki Meya wa Ilala pamojana Balozi wa Tanzania nchini Marekani mhe.Liberata Mulamula wakisubiria zamu zao za kuagana na Rais wa Marekani. |

Rais Obama na mkewe wakikwea pipa lao la Air Force One tayari kwa safari ya kurudi nchini Marekani mara baada ya kumaliza ziara ya siku Mbili nchini TANZANIA.

![]() |

Rais Kikwete ,Mama Salma na Kikwete,Naibu Waziri wa kilimo mhe Adam Malima (kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ,balozi wa Marekani hapa nchini Mhe.Alfonso lenhardt wakiwapungia mikono kuwaaga wageni wao ambao wamemaliza ziara yao ya siku mbili hapa nchini Tanzania baada ya k ufika jana na kufika ikulu kisha kuongea na Rais wa Tanzania Mhe.DKT JAKAYA KIKWETE na baada ya hapo alipata fursa ya kuongea na waandishi wahabari .



