Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » DUDE ANASWA NA DEMU MWINGINE

DUDE ANASWA NA DEMU MWINGINE


STAA wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amenaswa na demu mwingine aitwaye Mboni Mhando tofauti na mkewe anayeshi naye, Eva.
Dude na demu huyo aliyebainika kuwa ni msanii, walinaswa juzikati katika Hoteli ya Traventine Magomeni, jijini Dar wakijivinjari katika mikao ya kimalovee ambapo paparazi wetu alitumia kifaa maalum cha kupigia picha na kuwanasa bila wao kujijua.
Baada ya kuzinasa picha hizo, paparazi wetu alimvaa Dude na kumuuliza kulikoni agandane na demu huyo wakati ana mkewe nyumbani, alichomoa kuwa siyo demu wake bali ni msanii mwenzake eti wanapanga mipango ya kazi.
“Hapa tulikuwa tunapanga mipango ya kufanya filamu, huyu ni msanii tena wa siku nyingi sababu aliwahi kucheza kwenye Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu miaka ile,” alisema Dude huku akimsihi paparazi afute picha kama amekwisha piga.
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa