Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » , » BINTI WA MIAKA 15 AOZA SEHEMU ZA SIRI BAADA YA KUBAKWA NA KULAWITIWA MKOANI MTWARA

BINTI WA MIAKA 15 AOZA SEHEMU ZA SIRI BAADA YA KUBAKWA NA KULAWITIWA MKOANI MTWARA

Binti mmoja (jina tunalo) kutoka Mtwara aliyeletwa Dar es salaam kuja kufanya kazi amejikuta kwenye mateso makali baada ya kutelekezwa bila nauli na kukutana na fataki aliomshawishi na kumuweka kinyumba na kusababisha majanga hayo makubwa.
Akiwa na umri wa miaka kumi na tano (15) tu, alitolewa kwao Mtwara na kuletwa hapa Dar na dada mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Sophia kwa ajili ya usaidizi wa kazi za ndani.

Kwa maelezo yake ilitokea siku alimchapa mtoto wa bosi wake ndipo bosi alipokasirika na kufikia hatua ya kumtimua bila ya kumpa nauli ya kurudia kwao.

Alikutana na baba mwenye mke na watoto wa nne akamshawishi atampa maisha mazuri, akamweka kinyumba na kuanza kumtumia kimapenzi kinyume na maumbile. Kutokana na umri mdogo alionao,ilimsababishia kuharibika sehemu zake za siri na baba huyo na kumtelekeza baada ya kumtomlipia kodi sehemu aliyompangia chumba na majirani wa hapo ndio waliomsaidia.


Hivi sasa binti huyo ameoza sehemu zake za siri anamiminika usaha tu na amehifadhiwa hospitali ya Amana anakopatiwa matibabu na misaada midogo kama chakula.


Cha kusikitisha zaidi baada ya kupimwa kakutwa na Ujauzito wa miezi mitatu. na kapimwa virusi vya UKIMWI ambapo Vipimo vinatoka leo alhamisi kujua kama kaathirika au la.


 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa