Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » AONDOLEWA FUVU LA KICHA UPANDE MMOJA BAADA YA KUSHAMBULIWA NA RAFIKI YAKE .......MAPENZI NDIO CHANZO

AONDOLEWA FUVU LA KICHA UPANDE MMOJA BAADA YA KUSHAMBULIWA NA RAFIKI YAKE .......MAPENZI NDIO CHANZO

KUSHOTO: John Eccles baada ya kuondolewa sehemu ya fuvu lake. KATIKATI: Eccles akiwa hospitali baada ya kufanyiwa upasuaji wa fuvu lake. KULIA: Andrew Dodds.
Mtu mmoja alilazimika kuondolewa theluthi moja ya fuvu lake baada ya kuwa ameshambuliwa na rafiki yake wa zamani aliyegeuka mshindani wake katika mapenzi.
Wafanyakazi wa matibabu walilazimika kupachika kipande cha bati katika kichwa cha John Eccles baada ya kupondwa fuvu lake ukutano katika makabiliano hayo yaliyomwacha akiwa hajitambui kwa wiki mbili.
Mtu huyo mwenye miaka 35 alisema aliachwa kama alikuwa 'kagongwa na gari' wakati mwishowe alipozinduka hospitali hapo, ambako alilazimishwa kukaa kwa miezi sita.
Pale kwanza alipopata fahamu kufuatia tukio hilo dhidi ya rafiki yake wa zamani, Andrew Dodds, hakuwa akiweza kukumbuka kilichokuwa kimetokea.
Wanaume hao wawili walihitimisha urafiki wao wa zaidi ya miaka 20 pale Dodds alipoanza mahusiano na mpenzi wa Eccles na mama huyo wa binti yake.
Eccles aligonga kichwa chake ukutani baada ya kuwa amepigwa ngumi na Dodds nje ya klabu moja ya usiku mjini Consett, huko County Durham, Aprili mwaka jana, na kumwacha akiwa taabani.
Dodds alifungwa jela miaka mitatu Agosti, mwaka jana kwa kujeruhi kinyume cha sheria katika Mahakama ya Durham.
Eccles, ambaye anafanya kazi ya meneja wa zamu katika kituo cha kupumzikia, ameendelea kupata nafuu lakini anasumbuliwa na matatizo ya kupoteza kumbukumbu, kupooza upande wake wa kulia na kufanyiwa mazoezi ya viungo kusaidia aendelee kufanya shughuli zake za kawaida.
Akielezea kuzinduka kutoka kwenye shambulio hilo kwa mara ya kwanza, Eccles, mkazi wa Blackhill, karibu na Consett, alisema: "Sikufahamu kilichokuwa kikiendelea. Siwezi kukumbuka kilichotokea. Familia yangu ilibidi wanieleze."
Eccles alisema kwamba angeweza kufa kufuatia shambulio hilo lakini alisema alikuwa anaweza kurejea kufanya kazi.
Alisema: "Nina mkutano na watu wa afya sehemu za kazi wiki hii hivyo nitaona watakachosema, lakini ningependa kurejea kufanya kazi mapema iwezekanavyo.
"Nimekuwa nikielezwa inaweza kuwa miezi 18, inaweza kuwa miaka mitano au sita, lakini nataka kurejea sasa.
Eccles alitibiwa kufuatia kuvuja damu nyingi kwenye ubongo na akaendelea kukaa kwenye chumba cha uangalizi maalumu katika Hospitali ya Royal Victoria mjini Newcaste kwa miezi baada ya tukio hilo.
Sasa Eccles na mdogo wake, Mark mwenye miaka 32, wamekusanya takribani Pauni za Uingereza 1,000 kwa ajili ya kitengo hicho kufuatia usiku wa hisani kwenye Klabu ya Number One mjini Consett.
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa