Flora Mvungi katika pozi na mumewe Hamis Ramadhan ‘H. Baba’ siku ya harusi yao.
STAA wa filamu Bongo, Flora Mvungi amewashukia wabaya wake ambao wanaeneza maneno kuwa ndoa yake itadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Akizungumza na paparazi wetu, Frola alisema alipoamua kufunga ndoa na mumewe, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’ walishakaa muda mrefu na kuchunguzana, hawakukurupuka kuingia kwenye ndoa hivyo siyo rahisi kuachana kwa midomo ya washakunaku kama walivyotabiri.
“Wanikome! Wanaongea tena bila kujua watu tumetokea wapi, mimi na mume wangu tumetoka mbali mpaka kufikia hatua ya kuoana kwa taarifa yao ndoa yangu haitakufa ng’o,” alisema Flora.
“Wanikome! Wanaongea tena bila kujua watu tumetokea wapi, mimi na mume wangu tumetoka mbali mpaka kufikia hatua ya kuoana kwa taarifa yao ndoa yangu haitakufa ng’o,” alisema Flora.
Siku chache baada ya Flora kufanyiwa sherehe ya ‘send off’ wiki iliyopita, waliibuka baadhi ya wasanii walioichokonoa ndoa hiyo na kudai kuwa haitadumu zaidi ya mwaka mmoja.
Uchumba wa wanandoa hao ulidumu kwa miaka mitatu kabla ya kuchukua uamuzi wa kuoana.
Uchumba wa wanandoa hao ulidumu kwa miaka mitatu kabla ya kuchukua uamuzi wa kuoana.