Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » "KANGAMOKO" WAKAMATWA KWA KUJIUZA KINONDONI

"KANGAMOKO" WAKAMATWA KWA KUJIUZA KINONDONI

JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni, linalishikilia  baadhi ya wanenguaji wa kundi maarufu kwa  kucheza maungo yakiwa wazi ‘Kanga Moko na Laki si Pesa’, gazeti la Tanzania Daima la leo l ina hatimiliki ya hii habari.Watuhumiwa hao wamekamatwa sambamba  na watu wengi wanaofanya biashara ya kuuza miili yao, kufanya mapenzi hadharani
 na vitendo vya kishoga.Akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es salaam, Kamanda wa Polisi wa   Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema kuwa kundi hilo sambamba na  watu hao walikamatwa katika maeneo ya   Hoteli ya Travertine, Ambiance Club,   Kinondoni Makaburini, “Tumewakamata hao  wanaofanya mchezo maarufu wa  Kangamoko na Laki si Pesa na tayari  wanafikishwa mahakamani muda wowote  na msako bado unaendelea ili kudhibiti vitendo hivyo na michezo hiyo ya kangamoko au 
baikoko ambayo watu wengi wameilalamikia
  kutokana na mtindo wanaoutumia,” alisema.Kundi la kangamoko limekuwa likilalamikiwa
mara kwa mara kutokana na kucheza wakionesha maungo ya miili yao wazi na kuvaa nguo nyepesi wanazozimwagia maji.Kukamatwa wasanii wa kundi hilo kumekuja siku chache tu tangu walalamikiwe katikaBunge la Jamhuri ya Muungano kwamba wamekuwawakipotosha jamnii.

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa