Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » VIDEO QUEEN WA BONGO FLEVA AANGUSHA KILIO AKIDAI "KALOGWA" NA JACK WA CHUZ

VIDEO QUEEN WA BONGO FLEVA AANGUSHA KILIO AKIDAI "KALOGWA" NA JACK WA CHUZ

                         Mimah Mohammed  ‘Baby Candy’

 VIDEO Queen wa Bongo Fleva, Mimah Mohammed  ‘Baby Candy’ ameibuka na kueleza namna ambavyo aliugua malaria kali hadi kudaiwa kuwa amerogwa na shosti wake, Jacqueline Pentzel.

Chanzo makini kilituambia kuwa hivi karibuni nyota huyo alichanganyikiwa kwani majini huwa yanampanda kichwani mara kwa mara huku Jack  akidaiwa kuwa ndiyo chanzo cha matatizo hayo.

“Amewehuka kabisa, ukimuona utamuonea huruma na Jack ndiye anayedaiwa kumroga,” kilisema chanzo.
Baada ya habari hiyo kuvuja, paparazi wetu alimtafuta Baby Candy ambaye alikiri kuumwa pamoja kupata taarifa za uvumi kwamba Jack anahusika lakini yeye anamshukuru Mungu kwani ameshatibiwa hospitalini.
“Mimi na Jack bado tunaongea vizuri, niliamua kukaa mbali naye kwa sababu ya maneno mtaani, siwezi kusema alinifanyia kitu kibaya, nilikuwa nikisumbuliwa na malaria, nimetibiwa hospitali na sasa nimepona,” alisema.

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa