Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » USHAURI-"KWA NINI BOYFRIEND WANG ANAFANYA HIVI..?"

USHAURI-"KWA NINI BOYFRIEND WANG ANAFANYA HIVI..?"

Habari,

Kwanza kabisa, kwenye maelezo yangu nakuomba usionyeshe jina langu. Binafsi huwa naipenda sana blog yako, na kiukweli nimekuwa nikiifatilia sana.
Mimi ni Mtanzania ila kwa sasa naishi kwenye nchi moja iliyopo Barani Asia nikiwa nasoma.


Ipo hivi, nimekuwa kwenye mahusiano na boyfriend wangu kwa zaidi ya mwaka sasa, mtu ambaye naye yupo huku nilipo.
Wiki chache zilizopita amebadilisha status yake ya mahusiano kwenye Facebook, na kwa sasa inaonyesha yupo kwenye mahusiano na mwanamke mwengine na sio mimi.


Nilijisikia vibaya sana , nilipomuuliza aliniambia hakuna lolote linaloendelea kati yake na mwanamke huyo na cha msingi anasema nimuamini....
Ila hataki kuitoa hiyo status, anasema ataitoa muda mwingine sio kwa sasa. Kwa muda wa wiki sasa tumekuwa tukizungumza na kiukweli nampenda sana, sijui cha kufanya.
Tafadhali naomba ushauri, nachanganyikiwa....
Asante.

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa