RIPOTI ya Wiki leo imebaini kwamba pampasi (nguo za ndani za watoto) zina madhara kwa watoto na husababisha magonjwa ya kuambukiza kama yasipopatiwa tiba stahiki huweza kusabisha kifo.
Uchunguzi wa maripota wetu umebaini madhara hayo hutokea kwa kuwa pampasi zina uwezo wa kuhifadhi choo cha mtoto baada ya kujisaidia bila ya kupenya au kuvuja kwa upande wa pili kama ilivyo kwa nepi za kawaida.
Hivyo, hali hiyo huweza kusababisha magonjwa mbalimbali ya kuambukiza.
Ripoti ya Wiki ilifanya mahojiano na daktari wa magonjwa ya kina mama na watoto, Mr. Bujiku Constantine ambaye alieleza kuwa watoto wengi huugua magonjwa mbalimbali kutokana na matumizi ya pampasi, kama magonjwa hayo hayatatibika mara moja huweza kusababisha vifo kwa watoto.
Akifafanua baadhi ya magonjwa hayo, Dr. Bujiku alisema kuwa mtoto anayevalishwa pampasi huwa katika hatari ya kupata U.T.I (Urinary Tract Infections), Dermatitis (ugonjwa wa ngozi), Fangasi na Mabadiliko ya PH (kiwango cha tindikali) hasa katika sehemu za haja kubwa na ndogo, kutokana na unyevunyevu unaokaa kwa muda mrefu ndani ya pampasi hizo mara baada ya mtoto kujisaidia.
Akizungumza kwa msisitizo Dr. Bujiku alisema mtoto ambaye huvalishwa pampasi huwa katika hatari zaidi kuliko yule ambaye hutumia choo cha moja kwa moja.
“Magonjwa yote niliyoainisha hapo juu huweza kusababisha madhara tofauti kwa watoto ndani ya siku chache za matumizi ya pampasi.
“Kwa mfano U.T.I husababisha uchovu, maumivu ya mgongo, kuharibika kwa viungo vya uzazi, kuharibika kwa mfumo wa mkojo na kushindwa kufanya kazi kwa figo. Fangasi yenyewe, husababisha muwasho wa mara kwa mara, kuchubuka kwa ngozi na mara nyingine fangasi hao husambaa sehemu zote za siri za mtoto na kuingia ndani ya utumbo na kusababisha tatizo la fangasi tumboni.
“Dermatitis husababisha muwasho na harara katika sehemu za siri za mtoto hasa sehemu ambazo hufunikwa na pampasi hiyo. Hivyo kama magonjwa yote hayo hayatapatiwa tiba ya haraka, mtoto anayeugua anaweza kuwa katika hatari ya kifo,” alisema Dr. Bujiku.