Miongoni mwa washukiwa ambao wako mikononi mwa polisi ni raia wanne wa Saudi Arabia, na wengine wanne ni raia wa Tanzania.
Miongoni mwa waliokamatwa mpaka sasa ni wageni toka nje ya nchi ambao jeshi hilo limebainisha kama watalii.
Kumatatwa huko kunafuatia mlipuko uliotokea kanisani jijini Arusha jana, ambapo mpaka sasa watu wawili wanaripotiwa kufariki na wengine zaidi ya 60 wakiwa wamejeruhiwa.
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete amelaani tukio hilo na kuliita "kitendo cha kigaidi "