MREMBO Brandina Barthon (24), Jumatatu iliyopita alihukumiwa kwenda jela miezi 6 baada ya kupatikana na hatia kwenye kesi ya ukahaba iliyokuwa ikimkabili katika Mahakama ya Sokoine Drive (Jiji) jijini Dar.
Brandina alisomewa hukumu hiyo na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, William Mutaki ambaye alisema kutokana na ushahidi uliothibitika, mahakama hiyo inamhukumu kwenda jela miezi 6, ili liwe fundisho kwa wengine.Hukumu hiyo ilimfanya mrembo huyo kuchanganyikiwa na kuangua kilio lakini mheshimiwa hakimu aliamua kukazia hukumu yake bila ya kupepesa macho.
Wakati mwanamke huyo akiangua kilio, afande wa Jeshi la Magereza alimfikia na kumchukua kwa ajili ya kumpeleka kwenye Karandinga kuelekea Gereza la Segerea kuanza maisha ya jela.
Mbali na Brandina, mwanaume aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa mtuhumiwa huyo aliyekuwa akifuatilia kesi hiyo naye alimwaga machozi baada ya kutolewa hukumu hiyo.