Akizungumza na Exclusive Star, Batuli alisema kuwa hapendi kumhisi vibaya mtu yeyote juu ya tatizo hilo lakini hali hiyo inamkosesha amani kwani haelewi chanzo cha tatizo lake ni nini.
“Mimi kwa kweli sitaki kabisa kuweka imani tofauti ya kumhisi mtu vibaya ila najiuliza kwa nini nipandishe maruhani wakati wa kurekodi peke yake?” alisema Batuli.
Batuli aliongeza kuwa kinachomchosha zaidi hata akienda hospitali, huwa haonekani kama ana tatizo lolote, hali ambayo inampa mawazo zaidi.
“Namuomba Mungu anisaidie kwa maan
a hata tatizo lenyewe hospitali halionekani, inanitisha kweli,” alisema Batuli.

