Mwathirika wa utengenezaji upya viungo amejidunga sindano ya mafuta ya kupikia kwenye uso wake baada ya madaktari kugoma kumpatia silikoni zaidi.
Mrembo wa zamani Hang Mioku ameharibika kabisa sura yake kufuatia matibabu hayo ya urembo ya DIY.
Baada ya kujidunga usoni chupa nzima ya siliconi inayouzwa kienyeji mitaani, Hang aliamua kutumia mafuta ya kula ambayo yaliufanya uso wake wote kuvimba na kutisha.
Hali yanke mbaya ilioneshwa kwenye televisheni ya Korea na watazamaji walichangia maelfu ya Pauni kwa ajili ya kugharimia upasuaji wake wa kurekebisha sura yake.
Katika upasuaji wake wa kwanza kati ya 10 aliofanyiwa, madaktari waliondosha gramu 60 za silikoni, mafuta na vitu visivyotakiwa kutoka kwenye uso wake na gramu 200 kutoka shingoni mwake.
Hatahivyo, Hang bado ameharibika na anasemekana anatamani kama angerejea katika sura yake ya zamani.
Hang alianza mchakato wake huo akiwa na umri wa miaka 28 na kisha kwenda nchini Japan ambako alirudia matibabu hayo.
Haraka akanenepa kupita kiasi huku akiwa na ngozi nyororo na laini mno.
Madaktari ndipo wakagoma kumfanyia kazi yoyote zaidi baada ya uso wake kugundulika kuanza kuongezeka ukubwa.
Hatahivyo, aliweza kupata chupa ya silikoni na kujidunga sindano mwenyewe lakini wakati ikiendelea kufanya kazi aliishia kutumia mafuta ya kupikia.
Uso wake ulibadilika mno kiasi cha wazazi wake mwenyewe kushindwa kumtambua na watoto wa eneo hilo kuanza kumwita 'feni la sakafuni' sababu uso wake ulikuwa mkubwa mno kulinganisha na umbo lake dogo.
Upasuaji kadhaa uliolipiwa kutokana na michango uliweza kupunguza ukubwa wa uso wake na shingo lakini bado ameharibika kabisa sura yake.
Hivi karibuni mrembo huyo wa zamani alikuwa akifanya kazi kwenye duka la nguo kuukuu, linaloitwa The Beautiful Shop, na kupokea sadaka kutoka katika jimbo hilo.
Home
»
mitaa ya mbele
»
HAYA NDIO MATOKEO YA KUJIBADILISHA VIUNGO NA MAUMBILE ...!