Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » HALI NI MBAYA MKOANI MTWARA....MABOMU NA RISASI VIMETAWALA, HUDUMA ZA KIJAMII ZIMESTISHWA NA NYUMBA YA MWANDISHI WA HABARI WA TBC YACHOMWA MOTO

HALI NI MBAYA MKOANI MTWARA....MABOMU NA RISASI VIMETAWALA, HUDUMA ZA KIJAMII ZIMESTISHWA NA NYUMBA YA MWANDISHI WA HABARI WA TBC YACHOMWA MOTO

Hali ni tete na hakuna amani, mabomu ya machozi yanarindima muda huu na huduma zote za kijamii zimefunngwa hakuna usafiri, masoko, maduka na bar zote zimefungwa, daladala, Taxi na Bodaboda hazifanyi kazi.  
 
Kwa ujumla kinachoendelea ni mapambano makali kati ya Jeshi la polisi na wananchi wenye hasira wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato wa gesi ilihali nchi ikiwa haina sera inayosimamia nishati hiyo.
 
Kufuatia Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam ilihali Waziri wa Nishati akisoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na kusema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam Wananchi wa Mtwara walicharuka!
 
 Daraja la Mikindani limevunjwa hakuna mawasiliano Mtwara na Dar es salaam.
 
Baadhi ya Wananchi wamepora Silaha na wanazitumia kujibu mashambulizi ya Jeshi la Polisi (habari haijathibitishwa rasmi)
 
 Jengo la Ofisi ya CCM saba saba limechomwa moto. 
Lodge/Hotel (Shengena) inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa Jeshi la Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwaajili ya operation inayoendelea imechomwa moto.
 
Milio ya risasi na mabomu ndicho kinachosikika. 
Nyumba kadhaa  za watumishi  wa Serikali  zimechomwa  maeneo ya Shangani.

Ni magari ya FFU ndio yaliyopo barabarani nayo yanapata wakati mgumu kupita kwasababu ya mawe na magogo makubwa yaliyowekwa na Wananchi. 
 
Askari kadhaa wamekufa (habari hii haijathibitishwa rasmi)
Baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari kwakuwa wamepita jirani na gari yao.
 
Yadaiwa askari wengi waliokuja si wa Mtwara, wengi wametoka Masasi na Lindi. 
 
Ving'ora vinalia hovyo. Watoto wamefungiwa mashuleni walimu wamekimbia. 
 
Vituo vya Redio vya Mtwara havizungumzii hali hii ya hatari bali vinapiga Muziki pengine vinakusanya matukio na habari ya majanga haya ili Wananchi wayapate.
 
Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara, mpaka sasa takriban mabomu 20 na ushee yameshapigwa.
 
Jengo moja ambalo linadaiwa kumilikuwa na CCM limechomwa moto katika eneo la Majengo na daraja linalounganisha Lindi na Mtwara limevunjwa.


Mbali na hayo pia nyumba ya mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC)imechomwa moto.

Katika Mji wa Mtwara milio ya mabomu na risasi ndio inayosikika kila kona. Jeshi la Polisi linajaribu kuwadhibiti vijana  na watu wengine ambao wanafanya vurugu hizo.
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa