HABARI YA MLIPUKO-ARUSHA:
CHANZO KINASEMA, BOMU HILO LIMELIPUKA
WAKATI WAUMINI WA KANISA HILO LA
KATOLIKI WAKIENDELEA NA SHEREHE ZA
UZINDUZI WA KANISA HILO JIPYA JIJINI ARUSHA
TAARIFA ZINASEMA KUWA KUNA BAADHI YA
WATU WAMEJERUHIWA NA KUWAHISHWA
HOSPITALI KWAAJILI YA MATIBABU NA MPAKA
MUDA HUU HAKUNA ALIYEPOTEZA MAISHA
KUTOKANA NA BOMU HILO.
CHANZO CHA BOMU HILO INASEMEKANA KUNA
GARI AINA YA HIACE ILIFIKA KANISANI HAPO NA
KUSIMAMA BAADAE AKASHUKA MTU ALIYEKUWA
AMEVALIA VAZI MITHILI YA KANZU NA KURUSHA
BOMU HILO, BALOZI WA PAPA NCHINI NDIYE
ALIYEKUWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA
KANISA HILO JIPYA JIJINI ARUSHA NA
AMENUSURIKA KATIKA BOMU HILO ILA WATU
WENGI WAMEJERUHIWA
HIZI NI BAADHI YA PICHA KATIKA ENEO HUSIKA:
Hili ndo kanisa la olasiti....Mlipuko ulipotokea mapema asubuhi
Hii ni sehemu ambayo mlipuko umetokea asubuhi katika kanisa la olasiti hapa arusha
Mt.meru hospital....Ndugu na jamaa wakiwa nje ya hospitali kusubili taarifa za waliojeruiwa katika mlipuko uliotokea mapema asubuhi kanisani olasiti