Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » AFANDE SELE AANGUSHA KILIO JUKWAANI NA WASHABAKI NAO KUANZA KULIA

AFANDE SELE AANGUSHA KILIO JUKWAANI NA WASHABAKI NAO KUANZA KULIA


  MSANII mkongwe wa muziki wa bongo fleva  ambaye mpaka sasa anashikilia taji la mkali wa mashairi nchini Seleman Msindi'Afande Sele a.k.a Dume la Simba juzikati alizua taharuki kubwa kwa mashabiki waliofulika ndani ya kiwanja kipyacha Tanzanati Complex baada ya kuangua kilio jukwaani.Baada ya kuona hali hiyo waandaji wa shoo hiyo walipata jukwaani kwa kushirikiana na mabaunsa ambao kwa pamoja walimbembeleza msanii huyo bila mafaniki hali iliyosababisha baadhi ya mashabiki hasa wa kike nao kumsapoti kwa kuangua vilio vilivyovuma ukumbi mzima.
Afande Sele alipohojiwa na Audifacejackson alidai kwamba Kilio hicho kilitokana na
maudhui ya wimbo huo ambao ulimkumbusha  mambo mengi" Nikweli nimeshindwa kujizuia na
kuangua kilio nilipokuwa na imba wimbo wa Mkuki  Moyoni,kiukweli wimbo ule ulinikumbusha jambo
moja ambalo stoweza kulitaja kwa sasa"alisema Afande Sele baba wa watoto wawili Tunda na Asantesanaa


        Cheka akipanda jukwaani kumbembeleza rafiki yake kipenzi..Aidha baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya rafiki mkubwa wa Afande Sele bondi Francis Cheka'SMG' alipanda jukwaani na kubembeleza msanii huyo ambaye baada ya kubembezwa na Cheka alikubali kunyamaza kwa mashariti ya kutoendelea kuimba wimbo huo wa Mkuki Moyo ulioombwa na mashabiki wengi.Badala yake aliimba wimbo wa Darubini kali ambao alishirikiana kuimba na bondia Cheka aliyemudu vyema nafasi ya kiitikio iliyoimbwa na mdogo Dito na Mc Koba ambao kwa sasa wametengana na msanii huyo na kuunda kundi lao la watu Poli ,Cheka alikamua ile ile hali iliyoongeza radha ya burudani kwenye wimbo huo
 Baada ya Cheka kufanikiwa kumtuliza Afande Sele  waliimba wote wimbo wa Darubini Kali

                    Cheka na Sele wakikamua kwenye shoo shoo
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa