
Zenani Mandela

Makaziwe Mandela
Watoto wa rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela,wameamua kuchukua hatua za kuwaondoa wasaidizi wake watatu kutoka katika makampuni anayoyamiliki.
Makaziwe na Zenani Mandela wanadai kuwa watatu hao hawana haki ya kuwa kwenye bodi mbili za kampuni hiyo ambazo ni za thamani ya dola milioni 1.1. Kesi hiyo inakuja wakati kuna wasiwasi mkubwa kuhusu afya ya Mandela mwenye umri wa miaka 94.
Mandela aliondoka hospitalini baada ya kutibiwa ugonjwa wa mapafu pamoja na homa ya mapafu, na katika rekodi amelazwa hospitalini mara ya nne katika kipindi cha miaka miwili.

