Mjukuu wake aitwaye Omar ametoa taarifa kwa simu muda mfupi uliopita kuwa Bi. Kidude alikuwa amelazwa kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya sukarina uvimbe kwenye kongosho.
“Kwa ufupi alilazwa kipindi kirefu na baadaye akatolewa, lakini baadaye akaja kuendelea kuumwa tena tukampeleka hospitali tukawa tunampeleka kwenda na kurudi hapa juzi akaanza kuzidiwa tena tukampeleka hospitali moja inaitwa Keeni (???) Kwaajili ya matibabu zaidi na drip na vitu vingine lakini baadaye baada ya siku ya tatu mwenyezi Mungu akachukua roho yake,” amesema Omar. MSIKILIJE MJUKUU WA BIBI KIDUDE

