Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » KAULI YA DIAMONDI BAADA YA KULAUMIWA KUMDHALILISHA WEMA-'NI KWELI NILIMREKODI WEMA LAKINI SIWEZI KUMWOMBA MSAMAHA KWANI SIJAONA KOSA LANGU, MILIOCHUKIA KAZI KWENU'

KAULI YA DIAMONDI BAADA YA KULAUMIWA KUMDHALILISHA WEMA-'NI KWELI NILIMREKODI WEMA LAKINI SIWEZI KUMWOMBA MSAMAHA KWANI SIJAONA KOSA LANGU, MILIOCHUKIA KAZI KWENU'



Skendo iliyokuwa ikiendelea mtaani kuhusu msanii Diamond na tuhuma za kumrekodi aliyekuwa mpenzi wake wa zamani mwanadada Wema Sepetu, msanii huyo amekir kuwa ni kweli alifanya tuhuma hizo kwaajili ya kulinda penzi lake.

 “Hivi karibuni Wema amekuwa akinipakazia mbovu kwa mpenzi wangu Penny akiwa na leno la kutaka kuni haribia juu ya mimi na mpenzi wangu, nilichukia sana kwahiyo siku alivyoamua kunipigia simu ndipo niliamua kumrekodi ili kumsikilizisha Penny ambaye alikuwa haniamoni kabisa” Alifunguka Diamond.

Sauti hiyo ambayo ilitoka kwa Wema Sepetu ikiwa inambembeleza Diamond waweze kurudiana pamoja kwakuwa bado anampenda, Diamond amekiri kuirekodi hiyo sauti lakini amekana kuisambaza mitaani na hajui nani kafanya hivyo.

“Lengo langu kubwa ilikuwa ni kurekodi sauti hiyo  na kumsikilizisha Penny, sasa ambaye aliichukua na kuisambaza mitaani sijui ni nani, lakini hata mi sikujisikia vizuri nilipoisikia mitaani maana sikupenda hali iwe hivyo lakini ndo sina jinsi” aliongeza Diamond.

Baada ya kukiri kujutia, Diamond aliambiwa aombe msamaha Live ili Wema asikie ila alikataa na kusema hawezi kumuomba msamaha maana haoni kosa lake.
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa