MWIGIZAJI, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’ amewataka wasanii ambao umri wao umekwenda, wafanye maamuzi ya kuoana ili kujijengea heshima katika jamii.Dk Cheni alifunguka hayo juzikati katika hafla ya kumuaga Mfanyakazi wa Kampuni Global Publishers, Asteria Aaron pande za Posta, Dar ambapo baada ya kumaliza shughuli za ‘U-MC’, mwigizaji huyo alinaswa nje ya ukumbi akitoa hamasa hiyo kwa baadhi ya wasanii waliohudhuria huku akijipigia tenda ya ‘U-MC’. “Wasanii wanatakiwa kuoa na kuolewa kwa wale wa kike, ndoa ni heshima bwana. Wasisubiri miaka izidi kukatika, waoane na ikiwezekana wanipe dili ya kuwa MC si unajua tena mjini hapa!” alisikika Dk Cheni.