Uwoya akiwa na mumewe Ndikumana enzi hizo.
Akizungumza na gazeti moja la nchini Rwanda, Fatuma alisema kwamba hata ilivyotoka habari kuwa wifi yake Irene Uwoya amenaswa na Diamond alishtuka sana kwani yeye bado anaamini ndoa ya kaka yake ina uhai wa asilimia mia moja.“Nilishangaa sana kuona gazeti limeandika kuwa wifi yangu amenaswa na Diamond, mimi naamini ndoa ya kaka yangu bado ipo hai,” alisema Fatuma.
