Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » WEMA SEPETU ROHO MKONONI

WEMA SEPETU ROHO MKONONI

SEXIEST lady matawi ya juu kwenye sinema za Kibongo, Wema Sepetu ametishiwa kuvamiwa na watu wanaozaniwa kuwa ni majambazi.
Wema Sepetu.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mara baada ya Wema kutangaza kufungua ofisi kubwa ya kuzalisha filamu iliyopo Mwananyamala Komakoma, jijini Dar kimeibuka kikundi cha majambazi ambacho kimejipanga kumvamia ili kumpora fedha wakiamini anazo nyingi.
“Hicho kikundi kilimuona Wema akikatiza maeneo ya Kwa-Remmy, Sinza kikaanza kumjadili kuwa lazima wamfanyizie kwani sasa hivi ana fedha tena wakidai huwa anatembea nazo kwenye gari,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Niliposikia habari hizo nilikwenda kumtonya dada yake Wema anayeishi maeneo ya Kwa-Remmy ili amtahadharishe Wema katika mizunguko yake.”
Mtu wa karibu na Wema alifunguka kuwa mara baada ya kupewa taarifa hizo, mwigizaji huyo alitoa taarifa kwa maofisa wa usalama.

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa