MWANAFUNZI wa kiume mwenye umri wa miaka minane amemuoa mama mwenye umri wa miaka 61.
Kijana huyo Sanele Masilela alisimama mbele ya watu 100 na kufunga ndoa na Bi Shabangu, mama mwenye watoto watano .
Wawili hao walivalishana pete na kupeana mabusu motomoto Katika sherehe zilizofanyika Tshwane nchini Afrika Kusini, huku Sanele akidai mizimu ya mababu zake walimuamuru afunge ndoa hiyo.
Hata hivyo ‘wana ndoa’ hao hawakusaini cheti cha ndoa na wala hawaishi pamoja.
Selele alisema: “Nilimwambia mama yangu kuwa nataka kuoa, nina furaha kumuoa Hellen”.
Familia ya Selele imesema ndoa hiyo ni ya kiibada (kijadi) tu na wala siyo ya kisheria.
Mama wa Selele mwenye umri wa miaka 46 alisema babu wa mwanae alimtaka mjukuu wake aoe kabla hajafariki na akamchagua Hellen kwa kuwa alimpenda.
“Kwa kufanya hivyo mizimu ilifurahi. Kama asingetii basi jambo baya lingetokea kwenye familia."
WEWE UNAONAJE KUHUSI HABARI HII ? FUNGUKA HAPO CHINI KWA KUCOMMENT