Kajala akipandishwa kizimbani kusomewa hukumu.
Akitafakari.
Akitokwa na machozi baada ya kuhukumiwa.
Baba Kajala (kushoto) akishauriana jambo na wasanii wa filamu na maswahiba wa mwanaye.
MSANII Kajala Masanja leo ameachiwa huru baada ya kulipiwa faini ya shilingi milioni 13 na Wema Sepetu. Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na tuhuma za kutakatisha fedha haramu. Katika kesi hiyo, Kajala alihukumiwa kwenda jela miaka 5 au kulipa faini ya shilingi milioni 13. Faraji yeye amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 213.