Mtoto Sean Stewart wa nchini Uingereza, amekuwa baba mdogo pengine kuliko wote duniani baada ya mpenzi wake kujifungua wiki hii mtoto wa kiume mwenye afya.
Sean aliyetimiza miaka 12 mwezi uliopita, aliruhusiwa kutoenda shule ili kuwa pembeni ya mpenzi wake mwenye miaka 16, Emma Webster, wazazi wake Ray na Shirley, na mama yake Sean, Theresa. Alikuwa na miaka 11 na Emma miaka 15 alipopata ujauzito huo.
Yupo darasa la saba katika shule ya Margaret Beaufort.
Mwaka jana Sean alisema kuwa atakuwa bega kwa bega na Emma na mtoto wake pia. “I was shocked at first when I was told Emma was pregnant but I am all right about it now,” alisema Sean