Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » MSANII WA BONGO MOVIE LUPANGO KWA UJAMBAZI

MSANII WA BONGO MOVIE LUPANGO KWA UJAMBAZI

                                                                  Lungi Mwaulanga.
 STAA wa filamu za Kibongo, Lungi Mwaulanga hivi karibuni aliswekwa lupango katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar baada ya kuzushiwa kesi ya ujambazi na mpangaji mwenzake (jina tunalo).
Akizungumza na waandishi wetu, Lungi aliyesota mahabusu kwa siku mbili alisema hivi karibuni usiku wa manane aligongewa mlango nyumbani kwake na watu asiowafahamu, alipotoka alikutana na askari waliomchukua na kumwambia kwamba anatuhumiwa kwa ujambazi.
Hata hivyo, Lungi alisema kuwa baada ya kuwauliza askari ni wapi dada huyo amevunjiwa  au kitu gani alichoibiwa, askari walimbadilishia kesi na kumwambia kuwa amemtukana. Mpaka sasa, Lungi yuko nje kwa dhamana.

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa