![](http://4.bp.blogspot.com/-LSsaRwUfGDw/UVVdy11SoSI/AAAAAAAAArw/m_RhzEqUAcQ/s1600/Lulu-1.jpg)
Tukio hilo lilitokea Jumatatu iliyopita katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar ambapo wakati kesi ikiendelea, Lulu alisikika akiwaelekeza taratibu za mahakamani huku wenzake wakimtii.
“Sikilizeni niwaambie hapa mnatakiwa kunisikiliza mimi, hili suala litakwisha ndani ya muda mfupi hakimu atatoa hukumu, mimi najua siyo muda mrefu kuanzia sasa,” alisikika Lulu.