Waumini wa kanisa katoliki duniani jana wamepata Papa mpya baada ya kuchaguliwa na makadrinali katika zoezi la tano la uchaguzi baada ya mengine manne kushindwa kutoa moshi mweupe kuashiria habari njema.
Papa mpya ambaye ni raia wa Argentina Jorge Mario Bergoglio, askofu wa Buenos Aires ni mlatin wa kwanza kushika wadhifa huo wa kuongoza wakatoliki zaidi ya bilioni 1.2 duniani kote. Papa Francis ana umri wa miaka 76. Inadaiwa kuwa wakati Benedict XVI anachaguliwa alikamata nafasi ya pili. Alizaliwa mwaka 1986 huko Buenos Aires.
Viongozi mbalimbali duniani wametoa pongezi zao akiwemo Rais Barack Obama wa Marekani aliyemuita Francis, “mshindi wa maskini na wanyonge kati yetu.”
Akiwa kardinali, aliwahi kukwaruzana vikali na serikali ya Argentina ya rais Cristina Fernandez de Kirchner kuhusiana na kupinga kwake ndoa za jinsia moja na ugawaji wa dawa za kuzuia mimba.
Latin America ina waumini wa kikatoliki milioni 480. Kuchaguliwa kwa Bergoglio, makardinali wametoa ujumbe mzito kuhusu wapi mustakabali wa kanisa hilo utaelekea.
Home
»
mitaa ya mbele
»
HUYU NDIYE PAPA MPYA KWA WAKATOLIKI NA WASIFU WAKE