MSALA wa kudaiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 16, Sarah kwa takribani miezi minne umewaangukia watuhumiwa wawili, mtu na mdogo wake ambao Alhamisi iliyopita walifikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Kibaha, mkoani Pwani.
Watuhumiwa hao, Faida na Isaka wanatuhumiwa kumteka Sarah Novemba 25, mwaka jana kwa kumdanganya kwamba walikuwa na mzigo wa mama yake, hivyo wakamtaka awafuate wakampe ili ampelekee.
Inadaiwa kuwa Sarah alipowafuata walimfikisha hadi katika kibanda kimoja katika shamba wanalolilinda, lililopo Kibaha na kumtishia kumuua kwa kisu kama angepiga kelele.
Ndani ya kibanda hicho, Sarah anadaiwa kutengenezewa kishimo kilichozungushiwa matofali, kisha akawekwa kwa kujikunja kwa muda mrefu na kukosa mwanga wa kutosha.
Katika hali hiyo, Sarah alikumbana na joto kali lililombabua ngozi.
Taarifa zimesema kuwa Sarah alikuwa akipewa mlo mmoja kwa siku kila saa 7 usiku na alipoomba maji ya kunywa alipewa kidogo.
Mbali na hivyo, Sarah alidaiwa kuoga mara mbili tu katika miezi minne aliyoishi kama mateka katika kibanda hicho.
Inadaiwa kuwa, mtuhumiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Faida alikuwa akimtoa mdogo wake nje ya kibanda hicho na kupata fursa ya kumwingilia binti huyo kila alipojisikia kufanya hivyo.
Taarifa zinasema kuwa kitendo hicho kilimfanya Sarah kupata ujauzito na watuhumiwa hao walipogundua wakaamua kumtoa kwa njia za kienyeji.
Maelezo hayo ya awali yanasema kuwa watuhumiwa walichukua majani ya chai ya shilingi 500 wakayachemsha kisha wakamlazimisha kunywa.
Baada ya kutumia majani hayo, tumbo lilimkata Sarah, akaanza kutokwa na damu nyingi za mabongebonge kuashiria kufa kwa kiumbe kilichokuwa kimeanza kujitengeneza tumboni mwake.
Sarah alifanikiwa kutoroka alfajiri moja baada ya watuhumiwa hao kusahau kufunga mlango, akakimbilia msituni na kukutana na mtu aliyemfahamu ingawa awali mtu huyo alimuogopa kwa jinsi alivyokuwa.
Binti huyo aliongozana na msamaria mwema huyo hadi nyumbani kwa wazazi wake ambao walipigwa na butwaa walipomuona binti yao.
Binti alipelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Pwani, Tumbi na kukutwa akiwa na upungufu wa vitamini mwilini na baadaye kutoa taarifa polisi na watuhumiwa wakakamatwa.
Home
»
mtaa kwa mtaa
»
GAZETI LA RISASI-'MSALA ALIYEDAIWA KUMBAKA BINTI WA MIEZI MINNE KIZIMBANI'

