Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » VIDEO YA HIPHOP YA MSANII MTOTO WA MIAKA 9 YAZUA MJADALA

VIDEO YA HIPHOP YA MSANII MTOTO WA MIAKA 9 YAZUA MJADALA

poopyladies
Mtoto mwenye umri wa miaka 9, Luie Rivera Jr., ambaye jina lake la kisanii ni “Lil Poopy,” ameonekana kwenye video anazozipost online hususan kwenye mtandao wa YouTube, akicheza muziki na wasichana wakubwa kwa umri wake, akiendesha magari ya kifahari kama Ferrari na akirap maneno kama “coke is not a bad word.”
lil poopy
Katika video nyingine mtoto huyo anaonekana akicheza na msichana katika pozi chafu huku watu wakimtupia hela.
poopyladies
Idara ya polisi ya Brockton, Massachusetts, imewasiliana na ofisi inayoshughulikia masuala ya watoto na familia nchini humo baada ya kupokea simu nyingi kutoka kwa watu walioguswa kufuatia kuona video zake.
lil-poopy-584x350
Baba wa rapper huyo Luie Rivera ameajiri mwanasheria kujilinda na uwezakano wa kukamatwa kwa kosa la jinai.
Tazama video hii ya remix ya wimbo wa French Montana.



 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa