Simu hiyo imetengenezwa maalum katika maeneo ambayo umeme hakuna ama unasumbua lakini pia kama ‘backup phone’ pale zingine zinapozima.
Ikiwa inatarajia kuingia sokoni wiki kadhaa zijazo, Nokia 105 ambayo bei yake ni paundi 13, sawa na shilingi 30,000 za Tanzania pia ina tochi na FM radio.

