KAMA ilivyodhaniwa na wengi kwamba baba wa staa wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa atazungumzia dhamana ya Elizabeth Michael ‘Lulu’, kweli ameibuka na kusema yupo makini kufuatlia mwenendo mzima wa kesi hiyo ya kuua bila kukusudia. Hivi karibuni, Baba Kanumba alipiga simu kwenye dawati la vitukovyamtaa.blogspot.com kusema dhamana hiyo ya Lulu haimuumizi kichwa kwa sababu kila mtu ana haki ya kupewa dhamana kutokana na sheria ila yupo makini kufuatilia mwenendo wake.
Home
»
skendo mastaa
»
HII NDIO KAULI YA BABA KANUMBA JUU YA KUTOKA KWA LULU GEREZANI

