Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » HAYA NI MAONI YA WANANCHI JUU YA UBOVU WA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

HAYA NI MAONI YA WANANCHI JUU YA UBOVU WA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE



Jana matokeo ya kidato cha nne yalitangazwa na kuonesha jinsi wanafunzi hao walivyofeli ambapo waliopata daraja la kwanza ni 1,641, daraja la pili 6,453, daraja la tatu 15,426, daraja la nne 103,327 na waliopata sifuri wakiwa 240,903. Daraja la 1 hadi la 3 wavulana ni 16,342 na wasichana ni 7,178 pekee. 


Kupitia ukurasa wa Bongo5 wa Facebook ambao walikaribisha maoni kuhusiana na matokeo hayo. Nini kimesababisha wanafunzi wafeli kiasi hicho? Wadau mbalimbali walikuwa na haya ya kusema:

Nurdin Stambuli
Wanafunzi 23,520 tu ndio wamefaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu katika mtihani wa kidato cha nne wa mwaka jana. Hao ni asilimia 5.9 tu. Mwaka jana walifikia asilimia takriban 10 waliofaulu hivyo. Mwaka huu zaidi ya asilimia 60 wamepata daraja sifuri…toba!

Matokeo haya yanaanika wazi dosari katika mfumo wa elimu yetu. Msingi ukiharibika, ukuta utapasuka; na hata paa laweza ezuliwa na upepo mwepesi. Shule za sekondari hivi sasa hazichukui wanafunzi wenye sifa. Msingi wao wa kujifunza umeharibiwa tokea chekechea (hasa kwa kuwa wengi wameikosa, na walioipata wameipata kwa mapungufu makubwa) na shule za msingi.


Baada ya kuona kushuka kwa ufaulu kwa miaka kadhaa iliyopita; serikali ingeongeza alama za ufaulu; ili kuwapa shinikizo watoto wajifunze kwa bidii toka wakiwa shule za msingi. Kwa bahati mbaya sana, serikali ikaendelea kushusha alama ili kuchagua wanafunzi wakajaze nafasi sekondari; na ikawaondolea mtihani wa kidato cha pili, kwa kauli ambayo Profesa Jumanne Maghembe aliishadadia kuwa lazima mtoto anapoanza kidato cha kwanza amalize cha nne. Haya ndiyo matokeo tunayoendelea kuvuna mpaka sasa.


Kuna hitilafu kubwa sana katika usimamizi wa elimu yetu nchini, kiasi kwamba matokeo kadri yanavyokuwa mabaya yanakera na kuumiza nchi, wadau wa elimu, wanafunzi na familia zao. Iweje matokeo katika elimu yaendelee kuwa mabovu kuanzia darasa la nne, la saba, form two na form four kila mwaka? La, serikali inapaswa kuwajibika katika hili. Bila shaka viongozi na wasimamizi wa elimu yetu wamekosa mikakati. Hatuwezi kuboresha elimu bila kuboresha ufundishaji…na hatuwezi kuboresha ufundishaji bila KUWAWEZESHA WALIMU. Hilo nalo hawalijui? Angalau tuanzie hapo kwa sasa; tuwaheshimu na kuwawezesha walimu kufanya kazi yao.

Pamoja na umuhimu wa kuboresha elimu kuanzia kwa walimu; ni muhimu sasa watanzania; kuanzia wabunge na wadau wote wa elimu (wakiwemo wazazi, wanafunzi na walimu) tukadai mjadala mkubwa wa kitaifa kuhusu elimu. 

Hatuwezi kukwepa hili. Sera mpya ya elimu haijatoka mpaka sasa…ni muhimu sasa kuiomba na kuitumia fursa hii ili tujadiliane na kudai elimu tunayoitaka. Mheshimiwa James Mbatia alianzisha mada hii bungeni, lakini akakosa watu wenye mapenzi mema wa kumuunga mkono. 

Mheshimiwa Edward Lowassa naye aliliona hili mapema akasema iundwe tume ya wataalam kuuangalia upya mfumo wa elimu yetu kwa ngazi zote. Mawazo yake yakapita tu! Kuna kila dalili mbaya sasa katika elimu yetu ambapo hatuwezi kukwepa tena kuwa na mjadala wa kitaifa. Watakaoendelea kukosa elimu bora kila siku watakuwa ni watoto wetu wenyewe, hasa wanaosoma katika shule zetu za umma. 

Beatrice W Gatogo

Am a Kenyan and am greatly touched seeing just the no. of girls who passed in those exams……… I wish we awould all understand the importance of encouraging and putting all policies that support gal child education.no country or nation will move foward if they do not commit to promote education and more importantly emphasize on education for women! I love Tz just like it were my second home.


Rutaihwa Louis Aristides
Am very disappointed by the performance. the reasons given up here are all irrelevant and do not amount to the kind of failure the country has registered in the last year national exams. You are blaming phones, who buys the phones for the students? What do you do when a student has a phone? Social media like this one? No!!!!! Why, because you allow these students to miss use them. They even have access to pornography, sexual relationship i don’t believe it because i was in a serious relationship with my current wife when i was seating for senior four exams and we all excelled.


Ask yourself why some able parents are sending their children to study in Uganda and Kenya. Very few Kenyans and Ugandans come to study in Tanzania. My humble appeal to this government, education reforms are the way forward. Teacher motivations, could work it out, what about the parents what is your role in your child’s education? is it only to pay school fees and sit back? You are the cause of failure of your children.

Rashid Kiliza
1..Mapenzi ktk umri mdogo…2..Matumizi mabaya ya Mitandao kama facebook,Twitter,BBM,U-tube,Skype na Whats app wamekuwa addicted kiasi cha kushindwa kujipangia ratiba za kusoma baada ya kuitumia mitandao kutafuta vitu wanavyosoma wao hufanya vise versa…..3.Ufuatiliaji mdogo wa maendeleo ya Mwanafunzi pamojana malezi mabovu,….4.Nidhamu mbovu miongoni mwa wanafunzi na lenyewe ni kikwazo kama usharobaro na usharomaro kuna shule hizo miaka ya mwanzoni ya 2000 zilikuwa zinasifika kwa hilo lakini watu walikuwa kikazi zaidi….6..Tuition zisizo na mpangilio,Wanafunzi huenda kunyishwa sumu ktk Matuition ya kienyeji na kushindwa kuwaamini walimu wanaowafundisha darasani hatimaye kukosa muda wa kusoma..

Joyce Mmbaga
Tatizo ni kwamba serikali yetu haipo serious kwenye suala la elimu cause wakubwa wa nchi watoto wao wanasoma nje ya nchi, so ndio maana hawako makini na elimu ya hapa.

 Mimi nimeona kuna hizi shule za kata zipo Chanika huko, shule zina mandhari nzuri lkn ndio hivyo zipo mbali, serikali ikijenga hostel zile shule zikawa za boarding na kujenga nyumba za walimu itakuwa vizuri sana, maana mtoto akitoka nyumbani ni saa 11 asubuhi akifika shule ni saa 2 yuko hoi, hata mwalimu akifundisha haelewi ki2 then anatoka saa 8.30 akifika nyumbani hoi labda saa 12 au saa 1 atasoma saa ngapi? unadhani kuna kufaulu hapo, tunadanganyana tu, wanajidai wanachagua wanafunzi waende huko lkn hakuna ki2 kutokana na umbali, na kingine si kila mzazi mwenye uwezo wa kumpa mtoto nauli ya 1,500 kwa cku, inaleta vishawishi kwa wanafunzi wengine.
 
 
WEWE MSOMAJI ANDIKA MAONI YAKO PIA HAPO CHINI!
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa