Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » JAY DEE APATA WAGANGA 12 KWA KUMTIBU UGONJWA WAKE WA JINI MAHABA YANAYO MSUMBUA

JAY DEE APATA WAGANGA 12 KWA KUMTIBU UGONJWA WAKE WA JINI MAHABA YANAYO MSUMBUA

                                                 Mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’.
WAGANGA wanaodai kuwa ni wataalam na wana uzoefu wa kupambana na jini mahaba linalomsumbua Mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, wamejitokeza huku kila mmoja akiomba apewe nafasi ya kumtibu bure. 
Baada ya gazeti la ijumaa kuingia mtaani na stori inayoeleza jinsi jini mahaba anavyomsumbua Jide, watu wapatao 12 waliojitambulisha kuwa ni wataalam wa mambo hayo waliomba kuunganishwa na mke huyo wa Mtangazaji wa Radio Times FM, Gardner G. Habash huku wakiahidi kumtibu bila gharama yoyote.
Mmoja wa wataalam hao aliyejitambulisha kwa jina la Jumaa wa Magomeni, Dar alisema: “Nimesoma habari kuhusu Jide, mimi naweza kumtibu tena bure, mpe namba yangu na mwambie anipigie.”
Mwingine ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alisema: “Nimesikitika sana kusoma hii habari ya huyu msanii Lady Jaydee, kwa kifupi naweza kumtibia free of charge.”
Kufuatia maombi ya wataalam hao, mwandishi wetu alijitahidi kumtafuta Jide bila mafanikio lakini juzikati kupitia kipindi chake cha Diary ya Lady Jaydee alionekana akipewa matibabu na ustaadhi mmoja, mazingira yanayoashiria kuwa huenda mambo yametulia.
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa