Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » KIMENUKA MVOMERO MKOANI MOROGORO..VURUGU KUBWA YATOKEA LEO...MATUKIO KATIKA PICHA

KIMENUKA MVOMERO MKOANI MOROGORO..VURUGU KUBWA YATOKEA LEO...MATUKIO KATIKA PICHA


Askari wakijaribu kutuliza vurugu katika eneo la Mkindo wilayani Mvomero.
Gari la Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Wallace Karia lililovunjwa vioo likiwa kituo cha polisi Wami Dakawa.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka (kushoto) akiongea na wanahabari.
VURUGU kubwa zimezuka tena katika wilaya ya Mvomero leo baada ya wakulima kufunga barabara ya Turiani - Morogoro kwenye eneo la Mkindo. Wakulima hao walikuwa wakipinga wafugaji kuchoma nyumba zao kadhaa  sambamba na kuishinikiza serikali kuwaruhusu kulima kwenye bonde la Mgongolwa.
Katika vurugu hizo, askari mmoja amejeruhiwa katika paji na uso huku gari la Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Wallace Karia aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili SM 4503 likivunjwa vioo.
Pia waandishi wa habari wa TBC, ITV na Global Publishers waliofika eneo la tukio walipigwa mawe na wakulima.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alipohojiwa na waandishi nje ya kituo cha Polisi Dakawa alilaani kitendo kilichofanywa na wakulima hao na kulipongeza jeshi la polisi kwa kutumia busara wakati wa vurugu hizo licha ya kupigwa mawe.
Hadi mwandishi wa mtandao huu anaondoka eneo hilo bado barabara ilikuwa imefungwa.

-Gpl
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa