
Pichani ni mtangazaji wa kituo cha Television cha ITV Ufo Saro katika picha ya pamoja na Rais Jakaya Kikwete alipokutana na waandishi mbalimbali Ikulu Decemba 12, 2012
---------------------------------------
Kuna taarifa kwamba mtangazaji wa kituo cha Television cha ITV (Ufoo Saro) amepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya huko maeneo ya Kibamba leo Alfajiri na mama yake mzazi kuuliwa.---------------------------------------
Habari zaidi zinasema kwamba aliyefyatua Risasi hizo ni mchumba wa Mtangazaji huyo anayefanya kazi katika shirika moja la UN, ambaye baada ya tukio hilo naye alijipiga risasi na kujiua.
