Christian Bella.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Bella alisema kuna watu wamemzushia balaa hilo na amegundua wana chuki ya kutopenda maendeleo yake hivyo wamuache kwani yeye amelelewa katika familia ya kidini kamwe hawezi kutumia madawa ya kulevya.“Wabaya wangu walitaka kunishusha kimuziki ndiyo maana walinizushia skendo ya madawa hayo lakini wameshindwa. Tangu nizaliwe sijawahi kutumia madawa yoyote ya kulevya,’’ alisema Christian Bella.
Hivi karibuni, nyota huyo alipekuliwa kwa saa mbili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere baada ya kuhisiwa kuwa na madawa ya kulevya tumboni lakini aliachiwa baada ya kubainika hakuwa nayo.