Ingawa kuna ndugu wamekuwa wakijaribu kufanya kila kitu ni siri, lakini inaelezwa Mangwea alitumia madawa ya kulevya yaliyoisha muda wake na hata baada ya kifo chake ulizuka mzozo baina ya Watanzania wanaoishi nchini humo.
Rafiki yake Mangwea, M To The P, naye inadaiwa alitumia dawa hizo feki lakini hali yake inaendelea vizuri.
Mmoja wa Watanzania aliyekuwa wa kwanza kufika katika eneo la tukio.

“Unajua waliokuwa wanakaa nao (Mangwea na M To The P) hawakuwa waungwana, ndiyo maana baadhi ya Watanzania walikasirishwa, maana walipaswa wawaeleze kwamba sehemu fulani wanauza dawa za kulevya feki.
“Baadhi ya mateja wamethibitisha kwamba Mangwea na mwenzake (M To The P) walitumia madawa hayo feki, unajua mchanganyiko wake unakuwa kama sumu. Jamaa wanachanganya, wakati mwingine wanapatia na kuna kipindi inakuwa sumu. Watu kadhaa wamekufa hapa Jozi (Johannesburg).
“Sisi ambao tuko hapa Jozi tunaweza kuthibitisha kuwa Mangwea ameuawa na sumu iliyotokana na madawa feki. Angalia hata picha ya mwili wake kabla haujafanyiwa postmortem (uchunguzi), kulikuwa na mapovu ya madawa yaliyokuwa yamechanganyika na damu kuonyesha sumu ilikuwa tatizo.
“Huku (Afrika Kusini) watu hawana utu, waambie Watanzania wakija wasikurupuke tu,” alisema Mtanzania huyo aliyejitambulisha kwa jina la Joseph.
Juzi na jana mchana, Watanzania wanaoishi Afrika Kusini walikuwa wakihaha kupata rand 20,000 (dola 3,400) au Sh milioni 5.4 ili kununua jeneza.
“Fedha hiyo ni pamoja na suti, kuusafisha mwili, kuuweka kwenye jeneza pamoja na kuusafirisha hadi OT (Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo).”
Mangwea alikutwa amekufa chumbani katika moja ya vitongoji wanavyoishi watu wengi wa hali ya chini na kawaida jijini Johannesburg. Rafiki yake M To The P alikuwa anaendelea vizuri.
Akizungumza jana mchana kutoka Johannesburg, msanii Ruta Bushoke alisema walikuwa katika kikao eneo la Brixton alilokuwa akiishi Mangwea.
“Tuko hapa, Watanzania karibu wote tumekutana, tunasubiri kujua ripoti ya daktari itakuwa vipi, lakini tunaendelea kushughulikia mipango ya kumsafirisha marehemu.
“Unajua kuna mambo mengi lakini juhudi zinafanyika mwili uwe umefika huko Jumamosi, ila bado kuna mambo kadhaa ya kutatua, hapa ndiyo tunapambana,” alisema Bushoke aliyekuwa katika lebo moja na Mangwea ya Zizzou Entertainments.
Wakati tunakwenda mtamboni, M To The P alirejewa na fahamu na kitu cha kwanza alichokisema ni kuuliza Mangwea yuko wapi?
Taarifa zaidi mpaka jana jioni zilieleza kuwa Serikali ya Tanzania imekubali kuusafirisha mwili wa Mangwea utoa Afrika Kusini kuuleta Tanzania ambapo unatarajiwa kuzikwa keshokutwa mkoani Morogoro.
Awali kulitolewa ripoti ‘fake’ ya daktari, lakini ripori kamili kutoka kwa daktari ilitolewa jana jioni ambapo hadi tunaingia mitamboni ilikuwa haijawekwa wazi lakini watu waliokuwa karibu na marehemu waliliambia Championi Ijumaa kuwa inahusu madawa hayo yaliyosababisha kifo chake.