Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » MWANAFUNZI WA CHUO AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA "KISS" KWA MARA YA KWANZA

MWANAFUNZI WA CHUO AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA "KISS" KWA MARA YA KWANZA

Jemma Benjamin
Yapo matukio mengi yaliyotokea na yanaendelea kutokea katika karne ya 21 ambayo husikikitisha na yapo ya kushangaza kwa jinsi yalivyotokea, lakini hili pia ni moja kati ya yaliyowahi kushangaza na litaendelea kushangaza.

Wengi tunaamini kuwa mtu hupata mshtuko baada ya kupewa taarifa mbaya ama kushtuliwa kutokana na uoga wa kukwepa ajali. Lakini msichana Jemma Benjamini (18) alifariki kutokana na hisia alizopata baada ya kukiss kwa mara ya kwanza maishani mwake (First Kiss), April, 2009.

Kwa mujibu wa mtandao wa telegraph wa Uingereza, Msichana huyo muingereza ambae alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu, alipoteza maisha baada ya kupigwa busu na mwanafunzi mwenzake aliyefahamika kwa jina la Daniel Ross (21) nyumbani kwao na kijana huyo baada ya kutoka kwenye mtoko wa usiku kama marafiki.

Lakini katika mishemishe za kukaa pamoja kwa dakika kadhaa kwenye sofa wakibadilishana maelezo kadhaa walijikuta wakikiss taratibu, muda mfupi baada ya kiss hiyo Daniel alimuona mwenzake analegea taratibu huku macho yake yakiishiwa nguvu na kisha kutulia kabisa.

Hali hiyo ilianza kumtisha kijana huyo ambae anasema hawakuwahi kuwa na mahusiano ya mapenzi kabla, na hiyo ilitokea tu wakajikuta wanakiss.

“Haikuwa mahusiano ya mapenzi lakini tulikuwa tukikutana mara kadhaa kwa wiki, tulikuwa tunaelekea bar kupata chakula na tukarudi nyumbani kwa kuwa nilikuwa nimesahau credit card, tulikuwa tunaongea na tukajikuta tunakiss.

“Tulienda jikoni na baadae kwenye chumba cha kupumzika na Jema akakaa kwenye sofa,nikaanza kuona macho yake yanaanza kulegea ghafla kushuka, na mdomoni akaanza kutoa vijipovu vya mate kabla hajaanguka.”

Baada ya hapo alimpigia simu mama yake kisha akapiga simu kuomba msaada zaidi wa matibabu na ambulance ilifika na kumkimbiza hospital ambapo aligundulika kuwa tayari alikuwa ameshafariki. 

Ripoti ya uchunguzi ya daktari ilionesha kuwa hakukua na sababu zozote za kimatibabu zilizopelekea kifo chake. Na kwamba kifo cha msichana huyo kimetokana na matatizo yanayojulikana kama Sudden Adult Syndrome (SADS), tatizo dogo la moyo linaloaminika kuwauwa watu takribani 500 kila mwaka nchini uingereza.
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa