Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » MUIGIZAJI WA BONGO MOVIE ( KASHI) AFARIKI DUNIA LEO MCHANA

MUIGIZAJI WA BONGO MOVIE ( KASHI) AFARIKI DUNIA LEO MCHANA

 
Muigizaji wa filamu nchini Jaji Khamis (Kashi) amefariki dunia leo  mchana  katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.


Kashi amewahi kutamba na mchezo wa ITV, Tamu Chungu akiwa na wasanii wenzake kama Mzee Masinde,Samson na wengine.

Baada ya kupata habari hii, mwandishi wetu aliongea  na muigizaji mwenzake Monalisa ambae amethibitisha kutokea kwa msiba huo. Monalisa amesema alipata taarifa jana kwamba Kashi amelazwa hospitali akiwa amezidiwa kiasi cha kushindwa kuongea na hivyo kushindwa kujua nini kilikuwa kinamsumbua.

Naye Hemedy PHD ametweet: REST IN PEACE MUIGIZAJI MWENZETU JAJI KHAMIS KASHI….MUNGU AKULAZE PEMA PEPONI…MOVIE YA MWISHO TULICHEZA WOTE ILIKUA MATILDA!!Sad newz
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa