Home
»
mitaa ya mbele
»
KIJANA AJILIPUA MOTO BAADA YA KUKATALIWA KUONANA NA WAZIRI
KIJANA AJILIPUA MOTO BAADA YA KUKATALIWA KUONANA NA WAZIRI
Kijana mmoja nchini Jordan ambaye siku chache zilizopita alikataliwa kuonana na Waziri wa Ustawi wa Jamii wa Jordan na kuamua kujiteketeza, amefariki dunia hii leo kwenye hospitali ya serikali mjini Amman.
Kijana huyo yatima aitwaye Ahmad Rubain mwenye umri wa miaka 23 ambaye siku ya Alhamisi iliyopita alitaka kuonana na Waziri wa Ustawi wa Jamii na kumuelezea matatizo na hali ngumu ya maisha inayomkabili, aliamua kujiteketeza moto mbele ya jengo la wizara hiyo baada ya juhudi zake za kutaka kuonana na waziri kugonga ukuta.
Msemaji wwa Hospitali ya serikali ya al Bashir mjini Amman amesema kuwa, asilimia 90 ya mwili wa kijana huyo ilikuwa imeteketea. Hili ni tukio la tano la kujichoma moto katika kipindi cha miaka miwili nchini humo.
Ni miaka miwili na nusu sasa Jordan inakabiliwa na wimbi kubwa la maandamano ya wananchi wanaotaka yafanyike marekebisho ya kisiasa, kiuchumi na mapambano dhidi ya ufisadi nchini humo.