Askofu Kakobe
Katika mtandao wake wa Facebook, Askofu Kakobe amethibitisha kufanya safari hiyo akisema amefikia Marriot Hotel yenye ubora wa hali ya juu.Amesema mkutano wake wa kihistoria unafanyika kwa siku tatu, Juni 20 hadi 23 mwaka huu katika Kiwanja cha Rexall Centre ambacho huchukua watu 14,000 kwenye matamasha.

Kitanda anacholalia ni cha bei mbaya na ameandaliwa chumba maalum (presidential room) .
Askofu Kakobe pia anasaidiwa kutoa Neno na mhubiri maarufu wa Marekani, Don Moen ambaye anatajwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kuonesha ‘laivu’ miujiza ya Mungu.

Kakobe pia ametengewa siku moja, Juni 24 mwaka huu kukutana na wanandoa na atakula nao chakula cha usiku kisha atawafanyia sala maalum ili ndoa zao zidumu.
Jijini Dar, waumini wa Kakobe katika kanisa hilo lililopo Barabara ya Sam Nujoma wamekuwa wakikesha kumuombea kiongozi wao huyo ili apambane na maovu hasa mashoga wanaotajwa kuwa wanapinga mkutano wake wa kiroho katika Jiji la Toronto.
Katika Jiji la Toronto, mabango kuhusiana na ziara ya Askofu Kakobe yamewekwa katika mitaa mbalimbali na yameandikwa Toronto Miracle Healing Crusade hali inayofanya kufika kwake huko kuwa na msisimko wa kipekee.