Wolper
Kajala anakabiliwa na kesi ya kutakatisha fedha haramu kwa kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa kushirikiana na mumewe, Faraji Agustino.
kajala
Kwa mujibu wa mwigizaji mmoja maarufu wa kiume, tayari ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) na ujumbe kupitia mitandao ya kijamii umeanza kusambazwa kwa baadhi ya mastaa hao ambao kila mmoja anaonesha kuwa tayari kwa ishu hiyo ya kumuomba Mungu amsaidie Kajala.Ray
Mwigizaji huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe, alidadavua kuwa wanachotafuta kwa sasa ni mahali au nyumba ya ibada kwa ajili ya kufunga na kumwombea Kajala kuanzia saa 2:00 usiku hadi asubuhi.“Mwanzoni ilikuwa ni kuhamasishana tu kumkumbuka Kajala katika sala zetu za kila siku kama ilivyokuwa kwa Lulu (Elizabeth Michael), lakini sasa tumeona ni vema tukakutana kwa pamoja tumlilie Mungu ili hukumu yake imuendee vizuri,” alisema mwigizaji huyo na kuongeza:
“Yah! Kajala anatia huruma sana ndiyo maana kuna wasanii ambao ni watu wa karibu yake, wapo tayari kwa ajili ya mkesha wa maombi kama (Jacqueline) Wolper, Irene Uwoya, Patcho Mwamba, JB (Steven Jacob), Ray (Vincent Kigosi), Richie (Single Mtambalike), Dude (Kulwa Kikumba) na wengine wengi.”
Jb
Katika kesi hiyo iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, Kajala amesota Segerea kwa takribani mwaka mmoja ambapo sasa hatma yake itajulikana tarehe tajwa hapo juu.



